Mashabiki wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Uingereza, Arsenal, wamefunga barabara za kati kati ya jiji la Nairobi, siku ya Jumapili kusherehekea ushindi.
Mamia ya mashabiki hao wengi wao wakivalia jezi za Arsenal waliimba nyimbo huku wakipiga densi na kuwalazimu wenye magari kuyaegesha ili kutoa fursa kwa shamrashamra.
Wakiimba nyimbo we are the Champions yaani sisi ni Mabingwa ,mashabiki hao walikuwa wakifanya maandamano ya amani wamesitisha shughuli kati kati ya Jiji.
Msafara huo ulianzia katika eneo la Ambassador ,ambapo wengine walikuwa wakiuza jezi ,Vuvuzela na mitandio yenye nembo ya Arsenal, walipokusanyika kabla ya kuanza kuzunguka .
Sherehe za ushindi wa Arsenal pia zimeshuhudia maeneo ya Ngong Hills na Eldoret.

Mashabiki wengine wamepiga foleni ndefu kuzuru kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Hayati Raila Odinga katika eneo la Opoda Farm mapema Jumapili.
Arsenal watatawazwa mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza Jumapili,baada ya mechi ya kufunga msimu ugenini kwa Crystal Palace.
Ni mara ya kwanza kwa The Gunners, kushinda ligi Kuu Uingereza baada ya miaka 22.