AS FAR, kumenyana na Mamelodi fainali ligi ya Mabingwa Afrika

Timu zote zinawania Kombe la pili AS FAR, wakiibuka mabingwa mwaka 1985 nao Mamelodi, wakashinda mwaka 2016.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji AS FAR watakabiliana na Mamemodi Sundowns, katika marudio ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Jumapili mjini Rabat,Morocco.

Pambano hilo litang’oa nanga saa nne usiku katika uwanja wa Moulay Abdellah .

Mamelodi walishinda mkondo wa kwanza bao moja kwa bila wiki iliyopita.

Mshindi wa kombe hilo atatuzwa dola milioni 6 za Marekani, sawia na shilingi milioni 774 za Kenya.

Mabingwa watafuzu kwa fainali ya kombe la Super,mashindano baina ya mabara mwaka ujao na Kombe la Dunia mwaka 2029.

Timu zote zinawania Kombe la pili AS FAR, wakiibuka mabingwa mwaka 1985 nao Mamelodi, wakashinda mwaka 2016.

Share This Article