Uganda yathibitisha visa 3 vipya vya Ebola

Tom Mathinji
1 Min Read

Uganda imethibitisha visa vitatu vipya vya ugonjwa wa Ebola, na kufikisha idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo nchini Uganda kuwa kuwa 5.

Kupitia kwa taarifa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Ghebreyesus, alisema visa hivyo vipya viliwajumuisha mhudumu afya wa Uganda, dereva na raia wa DRC aliyesafiri kutoka mkoa wa Ituri nchini DRC.

Mkurugenzi Mkuu huyo aliwapongeza maafisa wa afya wa Uganda Kwa juhudi zao za kugundua, kufuatilia na kuwahudumia walipatikana na ugonjwa wa Ebola

WHO, ilisema inashirikiana kwa karibu na Shirika la Afrika la kuzuia na Kudhibiti magonjwa la  (Africa CDC) na washirika wa DRC na Uganda, Kudhibiti msambao, kuwasaidia waathiriwa na kuimarisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo.

Share This Article