Chandiru ashauri dhidi ya kuvujisha picha za utupu

Alisema kwamba hatua hiyo ni kinyume na maadili

Marion Bosire
1 Min Read

Jackie Chandiru mwanamuziki wa asili ya Uganda amepaaza sauti kuhusiana na mtindo unaoongezeka wa picha za utupu kuvujishwa mitandaoni.

Akizungumza kwenye mahojiano, Chandiru alisema kwamba hatua hiyo ni kinyume na maadili, akishauri wanawake watunze ufaragha wao na kukoma kukubali maombi ya kuhusika kwenye maudhui ya utupu.

Mwanamuziki huyo alilalamikia ongezeko la picha hizo mitandaoni akiongeza kusema kwamba wanawake hawafai kushurutishwa kutumia watu picha na video za uchi wao.

Alisisitiza kwamba yeyote anayetaka kuona mwanamke fulani uchi, anafaa kujenga uhusiano naye badala ya kuomba maudhui ya utupu kupitia simu za mkononi.

“Iwapo unataka kuniona uchi, lazima unichumbie. Kabla ya hapo tusalimiane kwa miezi kama sita alafu tujuane kwa muda kama wa mwaka mmoja” alisisitiza mwanamuziki huyo.

Chandiru pia alikosoa kile alichokitaja kuwa ni mbinu za udanganyifu zinazotumiwa na baadhi ya wanaume, akisema huwa wanashawishi wanawake kuamini kwamba kutuma picha za utupu ni kawaida na ni kuthibitisha upendo.

Kulingana na Chandiru, anayekupenda kwa dhati kamwe hatakuomba umtumie picha au video za faragha, kwa sababu angezingatia hatari zinazoweza kutokea endapo picha hizo zingevuja au kusambazwa.

Share This Article