Makonda asema angemwalika Snoop Dogg kusherehekea Bongo Flava

Serikali ya Tanzania inaandaa sherehe ya kuadhimisha miaka 30 ya muziki wa Bongo Flava.

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Paul Christian Makonda amezungumzia maandalizi ya maadhimisho ya miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva leo.

Makonda aliambia wanahabari kwamba alikuwa amepanga kumwalika mwanamuziki wa Marekani Snoop Dogg kama mgeni rasmi wa maadhimisho hayo lakini hakuweza kwa sababu ya ratiba ya msanii huyo.

Amesema tayari mazungumzo yalikuwa yameanza kati ya Serikali na usimamizi wa Snoop Dogg, lakini tarehe ya tamasha ikagonganga na kazi nyingine alizopanga msanii huyo.

Waziri huyo alisema kwamba serikali itaendelea kutafuta fursa za kuleta wasanii wakubwa wa kimataifa nchini humo ili waweze kushirikiana na wasanii wa Tanzania.

Maadhimisho ya miaka 30 ya Bongo Fleva, yatafanyika Julai 10, 2026, huko Mlimani City jijini Dar es Salaam, yakihusisha wasanii wakubwa na wa kihistoria wa nchi hiyo huku wengine wakitumbuiza mubashara.

Waziri Makonda alitoa mwaliko kwa raia wa Tanzania kuhudhuria hafla hiyo akielezea jinsi muziki umebadili maendeleo ya taifa hilo mapoja ya urithi.

Mikutano mingine sha kusherehekea muziki huo wa Bongo Flava imepangwa katika maeneo mengine 10 ndani ya Tanzania kutoa heshima kwa waanzilishi wa Bongo Flava na wanamuziki waliopo sasa.

Waandaji muziki na wasanii wa muziki wamekuwa wakiandaa nyimbo spesheli kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Share This Article