Deni la Msumbiji lapanda kwa asilimia 20

Mwaka 2025 pia ulikuwa mgumu kwa Msumbiji huku uchumi wake ukikua kwa asilimia 0.5 pekee.

Dismas Otuke
1 Min Read

Deni la umma la Msumbiji limepanda kwa asilimia 20, ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita kufikia mwaka jana.

Msumbiji ilifunga mwaka 2025 kwa deni la asilimia 72.23, ya pato la jumla la taifa hilo .

Shirika la kimataifa fedha (IMF) lilikuwa limeonya Februari mwaka huu kuwa taifa hilo linakabiliwa msukosuko wa kifedha kutokana na kupanda kwa deni la taifa.

Mwaka 2025 pia ulikuwa mgumu kwa Msumbiji huku uchumi wake ukikua kwa asilimia 0.5 pekee.

Hali hiyo ilisababisha upungufu wa fedha katika mifuko ya wananchi na kudumaza uwezo wao wa kununua bidhaa.

TAGGED:
Share This Article