Wanariadha 200 kushiriki majaribio ya mashindano ya Dunia kwa chipukizi

Hata hivyo Chama cha Riadha Kenya kimeweka masharti makali kwa wanariadha walioalikwa kwa majaribio hayo kikisisitiza kamwe hakitakubali udanganyifu wa umri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya wanariadha 200 wamealikwa kushiriki majaribio ya kitaifa ya kuteua timu itakayoshiriki mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 mwezi Agosti mwaka huu nchini Marekani.

Mwanariadha wa kwanza katika kila shindano wakati wa majaribio hayo yatakayoandaliwa uwanjani Nyayo kati ya tarehe 21 na 23 mwezi huu  atachaguliwa huku wa pili akiteuliwa na jopo la makocha.

Hata hivyo Chama cha Riadha Kenya kimeweka masharti makali kwa wanariadha walioalikwa kwa majaribio hayo kikisisitiza kamwe hakitakubali udanganyifu wa umri.

Kenya inalenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 mjini Lima,Peru, ilikomaliza ya tano kwa dhahabu 3,fedha 3 na shaba 1.

Share This Article