Amaan Ganatra apigwa jeki kwa mashindano ya Autocross

Ganatra aliye na umri wa miaka 17 ataendesha gari aina ya Mitsubishi Evo 9 .

Dismas Otuke
1 Min Read

Dereva chipukizi Amaan Ganatra amepigwa jeki anapojiandaa kwa msimu wa mwaka 2026 wa mashindano ya mbio za maagari maarufu kama Autocross ,yatakayofungua msimu Jumapili enep la Stoni Athi kaunti ya Machakos.

Ufadhili wa Ganatra kutoka kwa JCB,Royal Enfield Kenya,giant Godrej na kampuni ya pikipiki ya Uchina,Kove, umejiri wakati anapojiandaa kwa mashindano ya kufungua msimu Jumapili Mei 17.

Ganatra aliye na umri wa miaka 17 ataendesha gari aina ya Mitsubishi Evo 9 .

Msimu uliopita Ganatra aliibuka mshindi katika kitengo cha 4 wheel akiwa na mwelekezi wake Mudasar Chaudry.

Share This Article