Mashabiki wa tatu wa Senegal wameachiliwa huru jana Jumamosi, kutoka gereza moja nchini Morocco, baada ya kumaliza kutumikia kifungo cha miezi mitatu kwa makosa ya kuzusha vurumai wakati wa fainali ya AFCON kati ya timu yao na Morocco Januari 18 mwaka huu.
Wanaume hao watatu waliondoka katika gereza la Al Arjat 2 kaskazini mashariki mwa Rabat wakiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kuachiliwa huru.
Mashabiki hao waliskika wakiimba nyimbo za kuisifu Morocco, punde baada ya kufunguliwa .
Mashabiki wengine 15 wa Senegal wangali wanatumikia vifungo vya kati ya miezi sita na mwaka mmoja baada ya rufaa zao kukataliwa na mahakama mapema wiki hii.