Diana Wanza atwaa dhahabu ya tatu ya Kenya,Ghana

Wanza aliyekuwa alikamilisha mbio hizo za mizunguko 24 kwa dakika 31 sekunde 33.26,ikiwa dhahabu ya kwanza ya wanawake wa Kenya mwaka huu kwenye mashindanoi hayo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Diana Wanza alinyakua dhahabu ya tatu kwa Kenya, katika siku ya nne ya mashindano ya Riadha barani Afrika siku ya ijumaa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Accra nchini Ghana.

Wanza aliyekuwa alikamilisha mbio hizo za mizunguko 24 kwa dakika 31 sekunde 33.26,ikiwa dhahabu ya kwanza ya wanawake wa Kenya mwaka huu kwenye mashindanoi hayo.

Florence Niyonkuru wa kutoka Rwanda alishinda nsihani ya fedha sekunde 10.47 ,baadaye huku Arbaha Asefu wa Ethiopia akiridhia nishani ya shaba.

Kenya pia ilishinda medali ya kwanza ya mashindano ya uwanjani baada ya Belinda Obura, kunyakua shaba ya urushaji tufe.

Kenya ni ya pili kwenye jedwali la medali kwa  dhahabu 3,fedha 1 na shaba 3.

Ethiopia inaongoza kwa dhahabu 5,fedh 1 na shaba 5.

Share This Article