Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imesema inahitaji kitita cha shilingi bilioni 74, ili kuandaa Uchaguzi Mkuu ambao ni huru, wa haki na kuaminika.
Ilipofika mbele ya Kamati ya Bunge kuhusu Haki na Maswala ya Kisheria siku ya Jumanne, Kamati hiyo ilionya kuwa ina upungufu wa shilingi bilioni 33, swala linaloweza kuhujumu shughuli za uchaguzi hapa nchini.
IEBC ilisema hayo ilipowasilisha makadirio ya bajeti yake kwa mwaka wa kifedha wa 2026/2027.
Aidha, Tume hiyo imedokeza kuwa hadi sasa imepokea mgao wa shilingi bilioni 41.
IEBC inajiandaa kwa chaguzi ndogo mbili, moja katika eneo bunge la Emurua Dikirr Alhamisi Mei 14, 2026 na eneo bunge la Ol Kalou Julai 16, 2026.
Kiti cha eneo bunge la Emurua Dikirr kilisalia wazi kufuatia kifo cha Johana Ng’eno kupitia ajali ya helikopta, huku kile cha Ol Kalou kikiachwa wazi kufuatia kifo cha David Kiaraho alipokuwa akipokea matibabu.