Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetangaza kuwa idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini DRC, yamefikia watu 906 na vifo 223.
Ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo, ulio nchini DRC, pia umeripotiwa nchini Uganda.
Visa 125 vya maambukizi ya Ebola na vifo 17, vimeripotiwa nchini DRC ,katika maeneo ya Ituri,Kivu kaskazini na Kivu Kusini.
Visa saba vya maambukizi na vifo vitatu pia vimeripotiwa nchini Uganda, wagonjwa wote wakitokea DRC.