Naibu Rais wa Kenya Prof. Kithure Kindiki, amesafiri nchini Uganda kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni kwa muhula wa saba mamlakani.
Kindiki anamwakilisha Rais William Ruto, ambaye ni mwenyeji wa kongamano la siku mbili la Africa Forward, linaloandaliwa Jijini Nairobi.
Takriban Marais 30 na wajumbe 4,000 wanahudhuria kongamano hilo linaloandaliwa kwa pamoja na Kenya na Ufaransa.
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, pia anahudhuria sherehe hiyo ambayo inaandaliwa katika uwanja wa Kololo, Jijini Kampala.
Zaidi ya Marais na Viongozi 50 wa serikali wanahudhuruia uapisho huo wa Museveni, ambaye aliwaandalia dhifa ya jioni katika Ikulu ya Entebe.
Museveni anaapishwa kuiongoza Uganda kwa muhula wa saba mfululizo baada ya kuibuka mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu ulioandaliwa Januari 15, 2026.