Wydad washinda Casablanca derby

Wydad chini ya ukufunzi wa Mohammed Benchrifa, ni ya nne kwa alama 37.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wydad Athletic Club waliwashinda Raja Athletic Club, bao moja kwa bila katika derby ya Casablanca Jumamosi jioni.

Mechi  hiyo ya ligi kuu nchini Morocco, ilisakatwa katika uchanjaa wa Mohammed V mjini Casablanca.

Pambano hilo lililokuwa la raundi ya 20 katika ligi kuu nchini Morocco, lilichezwa bila mashabiki uwanjani kama tahadhari dhidi ya vurumai.

Joseph Bakasu, aliwafungia wekundu wa Casablanca, bao pekee na la ushindi kunako dakika ya 39, na kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa taji ya Botola Pro Inwi.

Raja wangali kileleni pa jedwali kwa alama 39, moja zaidi ya Maghreb de Fes, na mbili juu ya AS FAR, walio na mechi moja mkobani kila moja.

Wydad chini ya ukufunzi wa Mohammed Benchrifa, ni ya nne kwa alama 37.

Share This Article