Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines limetuzwa Shirika bora zaidi la Ndege barani Afrika. kwenye tuzo za APEX Passenger Choice Awards, 2026.
Tuzo hiyo inaashiria lengo kuu la shirika hilo kutoa huduma zilizoimarishwa kwa wateja wake, wakati wote wa safari.
Tuzo za APEX Passenger Choice, hutokana na huduma kwa wateja, ambao huelezea moja kwa moja jinsi walivyohudumiwa kwenye safari za ndege tangu wanapopokea tiketi hadi mwisho wa safari yao.
Kutambuliwa kwa Shirika la Ndege la Ethiopian na tuzo za APEX, kunaashiria kujitolea kwake kuhakikisha utoaji wa huduma za ubora wa hali ya juu kwa wateja na operesheni zilizoimarika.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Ndege la Ethiopia Mesfin Tasew, alisema ni fahari kuu kwa shirika hilo kupokea tuzo hiyo kutoka kwa wateja wake.
“Inaonyesha kujitolea kwa wafanyakazi wetu. Kutajwa Shirika bora la Ndege Afrika kunatupatia motisha ya kuimarisha viwango vyetu vya ubora na kukuza imani ya wateja wetu,’ alisema Tasew.