Serikali yapiga jeki Maendeleo ya Wanawake at 70 Mbao Sacco

Aidha, Katibu aliahidi kutimiza ahadi ya Rais Ruto ya kukipiga jeki chama hicho cha ushirika kwa kima cha shilingi robo bilioni ili kuanza kutekeleza shughuli zake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu wa vyama vya Ushirika Peter Kilemi, amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono kubuniwa kwa vya ushirika vingi zaidi nchini ili kuwawezesha Wakenya kiuchumi.

Kilemi amesema haya siku ya Alhamisi alipotoa cheti cha usajili kwa chama cha Ushirika cha Maendeleo ya Wanawake at 70 Mbao .

Aidha, Katibu aliahidi kutimiza ahadi ya Rais Ruto, ya kukipiga jeki chama hicho cha ushirika kwa kima cha shilingi robo bilioni ili kuanza kutekeleza shughuli zake.

Katibu katika wizara ya jinsia Anne Wang’ombe, alipongeza kubuniwa kwa chama hicho cha ushirika akisema kitawapa wanawake uwezo wa kiuchumi na kupunguza dhuluma za kijinsia ambazo hutokana hali ya kiuchumi ya wanawake.

Mwenyekiti wa Shirika la Maendelo ya Wanawake  Rahab Muiu, aliwarai akina mama kutumia fursa ya chama hicho cha ushirika kujiimarisha kiuchumi.

Share This Article