Uganda yaanza kuwarejesha makwao wahamiaji haramu 160

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Uganda imeanza zoezi la kuwarejesha makwao wahamiaji haramu 160, waliokamatwa jijini Kampala na viunga vyake.

Wizara ya mambo ya ndani nchini Uganda ilifanya msako Jumatatu wiki hii jijini Kampala, na kuwakamata raia hao wa kigeni ambao hawakuwa na stakabadhi wala vibali vya kuishi nchini humo.

Rai 23, walirejeshwa makwao Alhamisi Aprili 30, wakati wengine 18, wakisafirishwa Ijumaa Mei mosi, na kundi la mwisho litasafirishwa Jumatatu.

Wengi wa waliokamatwa ni wa kutoka Pakistan, wakiwemo wanawake 36,wengine wakitoka Bangladesh,India,Ghana,Myanmar,Ethiopia,Sri Lanka,Cambodia na Malasyia.

Serikali ya Uganda pia inachunguza watu wengine 67 raia wa Nigeria, ambao pia walikamatwa bila stakabadhi za kuishi wala  kufanya kazi.

Share This Article