Wanariadha 30 wa humu nchini walifanya mazoezi ya mwisho Ijumaa, kujiandaa kwa mbio za dunia za kupokezana kijiti zitakazoandaliwa baina ya kesho na Jumapili mjini Gaberone,Botswana.
Kenya itashiriki katika mbio za mita 100, kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti jinsia mchanyato,mita 100, kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti wanaume, na mita 400, kwa wanaume wanne kupokezana kijiti.
Fani nyingine kwa Wakenya ni mita 400, kwa wanawake kupokezana kijiti na mita 400, kwa wanariadha wanne jinsia mchanyato kupokezana kijiti.
Bingwa wa Jumuia ya Madola, Ferdinand Omanyala, anaongoza kikosi cha Kenya .
Kando na kuwania nishani mashindano hayo yanayoandaliwa Afrika, kwa mara ya kwanza yatatumnika kufuzu kwa mashindano ya Riadha Ulimwenguni, mwaka ujao mjini Beijing, Uchina.