Zanzibar wapata nyongeza ,Tanzania bara wakula hu

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita umeilazimu serikali ya Tanzania, kukosa kutekeleza nyongeza ya mshahara wakati wa siku kuu ya Leba Dei, wakati wafanyakazi wa Zanzibar wakiongezwa.

Rais Samia Suluhu Hassan  wa Tanzania,akiwahutubia wafanyakazi Ijumaa ,alisema serikali ilitumia pesa nyingi kukarabati na kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa wakati ghasia za Oktoba mwaka jana baada ya uchaguzi na mvua,kugharamia uchaguzi na kulipa madeni .

Rais Samia amesema asilimia 80, ya waajiri wa sekta binafsi wameongeza kima cha chini cha mshahara kufikia sasa, na kwamba serikali inaendelea kuzungumza na asilimia 20 iliyobaki ili walipe kima hicho ambacho ni TZSH 358,322.

Sherehe za maadhimisho ya siku kuu ya wafanyakazi duniani zimeandaliwa katika mkoa wa Njombe.

Wakati uo huo Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka TZSH 300,000, hadi TZSH 500,000, kwa mwezi.

Dkt. Mwinyi amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutekelezwa Januari 2027.

Share This Article