Maafisa wawili wa Polisi wafungwa jela kwa kosa la mauaji

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wawili wa Polisi wafungwa jela kwa kosa la mauaji.

Maafisa wawili wa polisi waliokabiliwa na mashtaka ya mauaji ya mshukiwa kwenye korokoro za kituo cha polisi cha  Nyamatoki kaunti ya Nyamira, wamefunga jela.

Wawili hao wanadaiwa kutekeleza mauaji hayo tarehe 19 Agosti, 2026.

James Ogwagwa Nyakina, mwenye cheo cha corporal, alihukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani, huku mwenzake Jackson Kirui Kipngeno mwenye cheo cha konstebo akihukumiwa miaka 10 gerezani.

Mahakama ilibainisha kuwa maafisa hao wawili waliokuwa wakifanya kazi katika kituo cha polisi cha Nyamatoki, walishirikiana kumuua Amos Kemosi Kereri.

Aidha, upande wa mashtaka ulisema kuwa wawili hao wakiwa katika zamu ya usiku pamoja na maafisa wengine wa polisi, walimkamata Amos Kemosi na kumpeleka kwenye kituo hicho cha polisi ambako walimjeruhi.  Alipopelekwa hospitalini kwa matibabu asubuhi iliyofuatia, alitangazwa kuwa amefariki.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 14, kuthibitisha kesi hiyo.

Share This Article