Mwanahabari mmoja apigwa risasi na kuuawa Kampala

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanahabari mkongwe nchini Uganda Joe Nam,amepigwa risasi na kuuawa papo hapo na mtu asiyejulikana akiwa  nyumbani kwake.

Mwanahabari huyo wa zamani wa gazeti la New Vision aliye na umri wa miaka 55, alipigwa risasi mapema  leo Jumapili katika eneo la Kawanda Cemntral,kata ya Nabweru katika wilaya ya Wakiso.

Ripoti za polisi zimearifu kuwa mshukiwa wa mauaji hayo alikuwa amevalia barakoa na alitoweka punde baada ya kumfyatulia risasi marehemu.

Nam aliuawa alipototoka nje kwenda maombi y na mkewe aliyeskia milio ya risasi alitoka nje na kumpata mumewe amefariki.

Kiini cha mauaji hayo bado hakijajulikana.

Share This Article