Rais wa Zanzibar Mwinyi akutana na Katibu Mkuu wa Afrika Mashariki

KBC Digital News
1 Min Read
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Stephen Patrick Mbundi

Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi akutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Stephen Patrick Mbundi, katika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha na kuaga rasmi.

Katika mazungumzo yao, Mwinyi alisisitiza kuwa wakati umefika kwa nchi wanachama wa EAC kuimarisha zaidi ushirikiano na kutumia kikamilifu fursa za maendeleo zilizopo kwa manufaa ya wananchi.

Mwinyi alimuhakikishia kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itaendelea kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya yetu.

Aidha, alieleza umuhimu wa kuangalia utekelezaji wa miradi ya pamoja itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika ukanda wetu.

Share This Article