Ratiba ya mechi za robo fainali kuwania taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, UEFA imebainika kufuatia kukamilika kwa michuano ya raundi ya 16 bora jana usiku.
Real Madrid walioibandua Manchester City watakwua na miadi na Bayern Munich katika hatua ya nane bora.
Arsenal walioitema nje Bayer Leverkusen kutoka Ujerumani watakuwa na kibarua dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno iliyowafurusha Bodo Glimt ya Norway.
Mabingwa watetezi PSG kutoka Ufaransa baada ya kuwabandua Chelsea sasa watakutana ana kwa ana na Liverpool iliyowalemea Galatasaray kutoka Uturuki.
Baada ya kuwatimua New Castle, Barcelona watavaana na Atletico Madrid katika robo fainali.
Mikondo ya kwanza ya robo fainali itasakatwa tarehe 7 na 8 mwezi ujao, huku marudio yakiwa wiki moja baadaye.