Uingereza yashikilia kuwa haitajiunga na vita vya Mashariki ya Kati

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ameshikilia kuwa taifa hilo halijajiunga na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Kwenye mkutano na wanahabari, Starmer hata hivyo alisema Uingereza ina meli za kivita zinazotekeleza utafutaji wa mabomu baharini katika eneo la Mlango-Bahari wa Hormuz

Kulingana na waziri huyo, Uingereza inashirikiana na washirika wake katika mpango wa pamoja wa kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, ili kufanikisha usafirishaji wa meli za mafuta.

Matamshi ya Starmer yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuihimiza Uingereza na nchi zingine kutuma meli za kivita katika Ghuba ili kusaidia kulinda njia ya usafirishaji, ambayo ni muhimu kwa usambazaji wa mafuta duniani.

Mlango Bahari wa Hormuz umefungwa  tangu vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vilipoanza, na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta.

Iran imetishia kushambulia meli zozote inazoona zina uhusiano na Marekani, huku pia kukiwa na hatari kutokana na mabomu ya baharini.

Share This Article