Mwanamitandao wa Kenya Diana Kemunto maarufu kama Shes Kemunto amefichua kwamba uhusiano wa kimapenzi kati yake na mwanamuziki Ian Okwemba Oure maarufu kama Iyanii.
Katika mahojiano na Alex Mwakideu, mrembo huyo alisema kwamba sababu moja ya kuvunjika kwa uhusiano wao wa kimapenzi ni hatua ya Iyanii ya kukosa kumhudumia alipougua.
Kemunto anasema alikumbwa na matatizo ya tumbo akalazwa hospitalini lakini Iyanii alikosa kumtembelea hospitalini kumjulia hali.
“Iyanii hakuwepo wakati nilikuwa ninamhitaji sana. Niliugua maradhi ya tumbo kwa sababu yake, nikajipeleka hospitali na hakuja kunijulia hali.” Kemunto alisema.
Mwanadada huyo anasema rafiki yake alimpigia simu rafiki ya Iyanii kumjuza kwamba Kemunto amelazwa hospitalini kwani Iyanii alikuwa hapatikani kwa simu.
Alipoondoka hospitalini baada ya kulazwa kwa wiki moja, anasema Iyanii alimtembelea nyumbani.
Kemunto anajikanganya katika suala zima la kuachana na mpenzi wake Iyanii kwani hivi maajuzi alihojiwa kwa njia ya simu na kituo kimoja cha redio ambapo alikanusha ripoti za kuachana na Iyanii.
Katika mahojiano hayo alisema kwamba yeye ametia saini upya mkataba wa mapenzi yao hata ingawa Iyanii atakosa kufanya hivyo.
Wakati walitangaza uhusiano wao wa kimapenzi mwaka jana, Kemunto alisema kwamba alimpa Iyanii muda wa miezi sita pekee afunge ndoa naye.
Anasema uhusiano huo uliodumu miezi mitano ndio uhusiano uliodumu muda mrefu zaidi maishani mwake ndiposa alitaka Iyanii amwoe haraka.