Bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge ametangaza kufungua msimu wake wa kushiriki mbio saba ulimwenguni atakapotimka mbio za Sanlam Cape Town Marathon.
Mbio za hizo zitaandaliwa Mei 24 mwaka huu.
Shindano hilo linalokuwa kila mwaka limewavutia wanariadha 27,000 kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Ingawa Kipchoge, mwenye umri wa miaka 41, alitangaza kustaafu kutoka mbio za kulipwa mwaka uliopita, bado anapania kushiriki marathon saba katika mabara tofauti kote ulimwenguni kwama nji ya kuhamasisha jamii.