Uwanja wa ndege wa Amboseli wafungwa kutokana na mafuriko

Dismas Otuke
0 Min Read

Uwanja mdogo wa ndege ulio katika mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Amboseli umefungwa kwa muda baada ya kuathiriwa na mafuriko.

Kwa kawaida, watalii hupaa kwa ndege kutoka uwanja wa Wilson hadi mbuga hiyo.

Uwanja huo umelowa maji kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikishuhudiwa tangu wiki jana.

Shirika la Wanyamapori nchini, KWS limeahidi kuufungua tena uwanja huo hivi karibuni kwa matumizi.

Share This Article