Bingwa wa Dunia wa Marathon Peres Jepchirchir apigwa marufuku kwa ulaji muku

Jepchirchir aliye na umri wa miaka 33, awali alikuwa ameshinda mbio za London Marathon mwaka 2024,Boston Marathon mwaka 2022 na New York Marathon mwaka 2021.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Dunia na bingwa wa zamani wa Olimpiki katika mbio za marathoni Peres Jepchirchir, amepigwa marufuku kwa muda baada ya kupatikana kuwa mtumizi wa dawa zilizoharamishwa aina ya EPO.

Jepchirchir ambaye ni mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia katika nusu marathoni alipatikana kuwa mtumizi wa dawa za EPO, aliporejea nchini baada ya kushinda mbio za Sydney Marathon mwezi Agosti mwaka huu.

Jepchirchir aliye na umri wa miaka 33, awali alikuwa ameshinda mbio za London Marathon mwaka 2024,Boston Marathon mwaka 2022 na New York Marathon mwaka 2021.

Pia Jepchirchir alishinda dhahabu ya Olimpiki mwaka 2021 mjini Tokyo,Japan.

Mwanariadha huyo ndiye wa hiviu punde wa haiba kuu humu nchini kupatikana kuwa mtumizi wa dawa za kututumua  misuli.

 

Share This Article