Aliyekuwa Msajili wa Idara ya Mahakama Anne Amadi ametwikwa majukumu mapya.
Hii ni baada ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, EACJ.
Amadi alikula kiapo cha utenda kazi wakati wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Wakuu wa Nchi uliofanyika mjini Arusha nchini Tanzania leo Jumamosi.
Naye alihudumu kama Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama kwa kipindi cha miaka kumi kabla ya kuondoka mapema mwaka 2024.
Muda mfupi baada ya kuondoka, aliwinda uenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, bila mafanikio.
Jitihada zake zikipigwa kumbo na kuteuliwa kwa Erastus Ethekon aliyeibuka mshindi wa wadhifa huo baada ya mahojiano yaliyohusisha watu kadhaa.