Wanaonufaika na mpango wa Inua Jamii wana siku tano kuchukua fedha zao

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu wa maswala ya kijamii na wakongwe Joseph Motari

Watu wote wanaonufaika na mpango wa kiinua mgongo kwa wazee wa Inua Jamii, wamepewa muda wa siku tano zaidi kuchukua pesa zao.

Katibu wa maswala ya kijamii na wakongwe Joseph Motari ameonya kuwa pesa hizo ambazo hazijachukuliwa na wenyewe, huenda zikarudishwa kwa wizara ya leba na maswala ya kijamii.

Agizo hilo linafuatia hatua ya serikali ya kuanza kulipa malipo ya mpango huo wa Inua jamii kupitia simu kutoka mtandao wa e-Citizen kuanzia mwezi Januari mwaka 2025.

“Wale ambao hawajachukua pesa zao za Iua Jamii wamepewa siku tano kufanya hivyo. Kama hawatazichukua kufikia Machi 15, 2025, tutachukulia kwamba hakuna watu kama hao,” alisema Motari.

Motari aliyasema hayo Jumanne usiku, akuzungumza na shirika la utangazaji nchini KBC.

Aidha katibu huyo aliongeza kuwa mpango wa Inua Jamii umeimarishwa zaidi, tangu utawala wa Kenya Kwanza ulipochukua usukani.

Alidokeza kuwa awali malipo yalikuwa yakitolewa kwa watu 194,000 ambao wamefariki, lakini sasa wameondolewa kwenya mfumo wa mpango huo.

“Tulipochukua usukani kutoka kwa utawala uliopita, tuliwaalika maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi EACC, kusaidia kuziba mianya iliyokuwepo. Maafisa hao waligundua kuwa malipo yalifanywa kwa watu 194 ambao tayari wamefariki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *