Rais Ruto afanya mazungumzo na Rais Museveni

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumapili alifanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, katika ikulu ya Entebbe.

Viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu maswala ya mataifa hayo mawili.

Rais Ruto alisema katika mazungumzo hayo waliangazia maswala ya biashara, usalama na kilimo.

“Kenya na Uganda zinajivunia ushirikiano dhabiti wa miongo kadhaa kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Rais Ruto.

Ziara yake inajiri wiki moja baada ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kukutana na Rais Yoweri Museveni.

Kenyatta alimtembelea Museveni katika wadhifa wake wa mshirikishi wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika mchakato wa kuleta amani nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Museveni alidokeza kuwa walikuwa na mazungumzo ya kufana huku akimshukuru Kenyatta kwa ziara hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *