Kenya yafuzu kwa mashindano ya Dunia mbio za mita 400 kupokezana kijiti

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu mbili za Kenya za mbio za mita 400 kwa wanaume wanne kupokezana kijiti na ile ya mita 400, kupokezana kijiti mseto zilijikatia zilifuzu jana kwa mashindano ya Riadha Duniani yatakayoandaliwa Septemba mwaka huu.

Kikosi cha Kenya cha mita 400 wanaume kilichowajumuisha Zablon Ekwam,Boniface Mweresa,Brian Tinega na Kevin Kipkorir, ilifuzu kwa mashindano ya dunia baada ya kumaliza ya pili katika mchujo wa nne kwa kutumia dakika 3 nukta 88.

timu ya mita 400 mseto wa kupokezana kijiti kikiwajumuisha David Kariparante, Mercy Okoth,Mercy Chebet na Kevin Kipkoech ilichukua nafasi ya tatu katika mchujo kwa muda wa dakika 3 sekunde 13.41,ukiwa muda wa kasi msimu huu.

Aidha timu zote mbili zilifuzu kwa fainali kwa mbio za Dunia za kuopokezana kijiti zinazoendelea mjini Guanzhou,China.

Share This Article