Mabingwa watetezi Argentina watakumbana na Uhispania katika fainali ya Kombe la Dunia makala ya 23 Jumapili usiku kuanzia saa nne uwanjani New York, New Jersey Marekani.
Fainali hiyo ambayo ni mechi ya 104 ya dimba la mwaka huu itahitimisha burudani ya siku 37 za kindumbwendumbwe hicho, ambacho kimekuwa kikiendelea tangu Juni 11, katika viwanja 16 vilivyokuwa katika miji 16 ya mataifa ya Mexico,Canada na Marekani.
Itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kumenyana kwenye fainali za Kombe la Dunia ,baada ya Argentina kuibwaga Uhispania, magoli 2-1,katika mechi ya makundi mwaka 1966.
Timu zote mbili zinajuvunia kutopoteza mechi katika mashindano ya mwaka huu.
Kuelekea fainali Argentina waliotwaa ubingwa wa mwaka 2022,waliongoza kundi J kwa kushinda mechi zote tatu dhidi ya Algeria,Austria na Jordan.
Katika raundi ya 32 Argentina walihitaji muda wa ziada kuwashinda Cape Verde 3-2 na kuwatitiga Misri pia 3-2 katika awamu ya 16 bora.
La Abisceleste wanavyojulikana Argetina waliibandua Uswizi 3-1, kupitia muda wa ziada na hatimaye kutoka nyuma na kuwaangusha Uingereza 2-1 katika hatua ya nusu fainali.
Kwa jumla Argentina wamefunga mabao 17 na kufungwa 7 huku Lionell Messi akitikisa nyavu mara 8.
Upande wa Uhispania almaarufu La Roja,walitoka sare tasa na limbukeni Cape Verde, katika kundi H,kabla kuwazabua Saudi Arabia na Uruguay na kuongoza kwa pointi 7.
Uhispania iliikomoa Austria 3-0 katika awamu ya 32 bora na kuwatimua Ureno 1 bila jawabu katika 16 bora .
Katika robo fainali Uhispania iliwapiga Ubelgiji 2-1 na hatimaye kuwazima Ufgaransa 2-0 katika nusu fainali.
Kwa jumla Uhispania imefunga mabao 13 na kufungwa moja.
Aidha,miamba hao wawili wamechuana katika mechi sita za kirafiki Uhispania wakishinda nne nao Argentina wakaibukia mara mbili.