Mwimbaji wa Mali, Amadou Bagayoko afariki

Hata hivyo, Amadou aliyepoteza uwezo wa kuona alijiunga na taasisi ya watu wasio na uwezo wa kuona mjini Bamako mwaka 1975.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwimbaji mashuhuri wa Mali, Amadou Bagayoko, alifariki jana akiwa na umri wa miaka 70 baada ya kuugua kwa muda.

Kulingana na familia yake, Bagayoko, ambaye aliunda bendi pamoja na mkewe na kuipa jina la Amadou & Mariam, alizaliwa mjini Bamako Oktoba 24 mwaka 1954.

Amadou alianza kucheza muziki akiwa na umri wa miaka 10, na baina ya mwaka 1974 na 1980, alikuwa mwanachama wa bendi ya Ambassadeurs du Motel, mojawapo wa bendi maarufu nchini Mali iliyomshirikisha msanii Salif Keïta .

Hata hivyo, Amadou aliyepoteza uwezo wa kuona alijiunga na taasisi ya watu wasio na uwezo wa kuona mjini Bamako mwaka 1975.

Website |  + posts
Share This Article