Rais Trump atangaza vita vya kibiashara na washirika wake

Trump ametangaza ushuru mpya wa forodha wa asilimia 20 kwa bidhaa za kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU), China ikiongezewa ushuru mpya wa asilimia 34 kuongozea kwa ushuru wa awali wa asilimia 20.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuanzishwa rasmi kwa viwango vipya vya ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka mataifa ya nje kwa kile kinachoonekana kama vita vya kibiashara na washirika wake wakuu.

Akihutubia taifa jana Jumatano, Trump alitangaza nyongeza ya ushuru wa chini kwa asilimia 10, kwa bidhaa zote kutoka mataifa ya kigeni huku zaidi ya nchi 60 zikitarajiwa kuathiriwa wakati agizo hilo litakapoanza kutekelezwa tarehe 9 mwezi huu.

Trump ametangaza ushuru mpya wa asilimia 20 kwa bidhaa za kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU), China ikiongezewa ushuru mpya wa asilimia 34 kuongozea kwa ushuru wa awali wa asilimia 20.

Hii ina maana kuwa bidhaa zinazoingia Marekani kutoka China, zitalipiwa ushuru wa asilimia 54.

Bidhaa za kutokea Mexico kuingia Marekani zitatozwa ushuru wa asilimia 25 .

Hali hii inatarajia kuyasukuma mataifa hayo yaliyoathiriwa pia na kupandisha ushuru kwa bidhaa za kutokea Marekani, hali ambayo itaathiri vibaya chumi za mataifa husika.

Website |  + posts
Share This Article