Wanariadha zaidi ya 1,000 kushiriki mkondo wa nne Nakuru

Fani 11 zitakashirikishwa, zikiwemo mita 100, 200, 400, 800, 1,500, 3,000 kuruka viunzi na maji, 5,000 na mita 10,000 matembezi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha zaidi ya 1,000 watashiriki mkondo wa nne wa mashindano ya Chama cha Riadha Kenya, utakaoandaliwa kati ya Ijumaa na Jumamosi hii, Aprili 4 na 5, uwanjani Afraha, Nakuru.

Ni mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kwa mashindano ya riadha kuandaliwa katika uwanja huo unaofanyiwa ukarabati.

Fani 11 zitakashirikishwa, zikiwemo mbio za mita 100, 200, 400, 800, 1,500, 3,000 kuruka viunzi na maji, 5,000 na mita 10,000 matembezi.

Aidha, kutakuwa na mashindano ya ndani ya uwanja kama vile urushaji nyundo (hammer throw), urushaji kijisahani (discuss), na kuruka mapana (long jump).

 

Website |  + posts
Share This Article