Mpenzi wa 2Baba aashiria kwamba huenda walifunga ndoa kisiri

Alichapisha video fupi mitandaoni ambapo anaonyesha pete ya ndoa inayoaminika kuwa ghali kwani ina vipande vya almasi.

Marion Bosire
1 Min Read
Mpenzi wa 2Baba.

Natasha Osawaru mbunge katika bunge la jimbo la Edo nchini Nigeria na ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki 2Baba ameashiria kwamba huenda walifunga ndoa kisiri.

Haya yanatokana na video fupi aliyochapisha mitandaoni ambapo anaonyesha pete ya ndoa inayoaminika kuwa ghali kwani ina vipande vya almasi.

Osawaru hakusema lolote kuhusu video hiyo lakini wanamitandao nchini Nigeria walitambua haraka kwamba alikuwa anatambulisha pete yake ya ndoa.

Binti huyo ambaye anaaminika kuvuruga ndoa ya 2Baba na mkewe Annie Macaulay amekuwa akichapisha video na picha za kuashiria kuimarika kwa uhusiano wake na mwanamuziki huyo.

Siku chache zilizopita, Natasha aliondoa jina la babake Osawaru kwenye utambuzi wake wa mtandao wa Instagram na kuweka jina la 2Baba la Idibia ambalo ameandika kwa herufi kubwa.

Kwa uande mwingine, Annie anaonekana pia kupona kutokana na maumivu ya moyo yaliyotokana na tangazo la ghafla la 2Baba mitandaoni kwamba walikuwa wameshatengana na wanaendeleza mchakato wa talaka.

Annie amerejea mitandaoni ambapo alifuta picha zote za awali na chapish la pekee jipya ni la kushukuru wote ambao wamekuwa wakisimama naye wakati anapitia magumu.

Website |  + posts
Share This Article