Harambee Stars kazi ipo leo dhidi ya wenyeji Pemba mshindi kuingia fainali

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya ,Harambee Stars itashuka ugani Gombani leo kisiwani Pemba, dhidi ya wenyeji,ikihitaji ushindi ili kufuzu kwa fainali ya  kombe la Mapinduzi mwaka 2025.

Kenya chini ya uongozi wa mwalimu wa muda Francis Kimanzi walifungua michuano hiyo kwa kutoka sare ya bao 1 dhidi ya Burkina Faso,  kabla ya kuwazidia maarifa Tanzania magoli mawili bila jawabu.

Upande wao Burkina Faso walitoka sare na Kenya,kabla ya kuwashinda Pemba goli moja kwa bila na kuwabwaga Tanzania bara mawili bila jawabu.

Burkina Faso wanaongoza kwa alama 7 ,wakifuatwa na Kenya kwa alama 4 wakati wenyeji wakiwa na alama 3.

Timu mbili bora zitapambana katika fainali ya Januari 13.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *