Serikali kujenga mabwawa zaidi kuunga mkono kilimo North Rift

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri wa Maji Eric Mugaa akiwa na Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii

Serikali ina mipango ya kujenga mabwawa zaidi kwa lengo la kupiga jeki shughuli za kilimo katika eneo la North Rift.

Waziri wa Maji Eric Mugaa amesema uwezo wa kilimo wa eneo hilo haujaafikiwa kikamilifu kutokana na uhaba wa maji.

“Tunaangazia tatizo hili kwa kujenga mabwawa zaidi ambayo yataongeza kiwango cha ekari kutoka ekari za sasa 6,000 hadi 9,000,” alisema Mugaa.

Waziri huyo aliyasema hayo leo Jumatano alipokagua miradi ya maji katika kaunti ya Uasin Gishu.

Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo katika eneo hilo kuanzia kesho Alhamisi.

Waziri Mugaa amesema kutotegemea mvua kufanya shughuli za kilimo kutaifanya nchi hii kuwa na chakula cha kutosha, kubuni nafasi zaidi za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *