Vijana wajenge uwezo wao kwenye siasa, mbunge wa Ugenya ashauri

Francis Ngala
2 Min Read

Mbunge wa Ugenya David Ochieng ametoa mwito kwa vijana kutoa sauti zao kupitia upigaji kura ili kuendeleza ajenda zao za kisiasa na kiuchumi.

Kwa mujibu wa David Ochieng, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Movement for Democracy and Growth Party, siasa ndio inayoamua maisha hasa uchumi wa vijana hivyo hawapaswi na hawawezi kukwepa siasa.

Aliwashauri vijana kushiriki kikamifu katika mchakato wa siasa, uchaguzi na uongozi kwani kwa namna yoyote mambo hayo hugusa na kuathiri maisha yao. Hata hivyo, Ochieng aliwataka vijana kutafuta vitambulisho pamoja na kadi za kupiga kura, akibainisha kuwa hati hizo mbili ni vyombo muhimu vya kutekeleza haki zao za kidemokrasia na kusikilizwa sauti zao.

“Kama unataka mabadiliko yatokee unavyotamani lazima ushiriki kwenye siasa katika ngazi zote, iwe ni kupitia uhamasishaji au kwa kugombea nyadhifa ili uchaguliwe,” alisema mbunge huyo.

Ochieng alisema kuwa kama ilivyoshuhudiwa wakati wa maandamano ya hivi majuzi ya vuguvugu la Gen-Z, vijana wanaweza kuwa nguvu ya kuzingatiwa ikiwa wamejipanga vyema na kuonyesha ari katika kutekeleza ajenda zao.

Mbunge wa Ugenya David Ochieng akiwakabidhi washindi tuzo zao katika hafla ya ‘KUSA AWARDS’ iliyofanyika usiku wa kuamkia Leo chuo kikuu cha KU

Mbunge huyo alisema haya katika Chuo Kikuu cha Kenyatta wakati wa hafla ya utoaji tuzo ya kila mwaka ya chama cha wanafunzi wa taasisi iliyopewa jina la “KUSA Awards”, ambapo alikuwa mgeni wa heshima.  Hafla hiyo ya kupendeza ilifanyika katika ukumbi wa michezo chuo hicho.

 

francis ngala

I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *