Serikali yaanza majadiliano kuwanusuru Wakenya waliotekwa nyara Myanmar

Wakenya 23 walikuwa miongoni mwa watu 260 waliokolewa na kuruhusiwa kuvuka mpaka baada ya mpaka kufunguliwa kuokolewa kutoka kwa mikono ya maharamia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Kenya imeanza mazungumzo na serikali ya Thailand ili kuwarejesha nyumbani Wakenya 64 walio miongoni mwa watu 7,000, walionusuriwa na maafisa wa polisi wa Myanmar kutoka kwa biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu.

Taarifa kutoka kwa idara ya Wakenya walio ughaibuni imesema wanazungumza na serikal ya Thailand, ili kufungua mpaka na kuwaruhusu Wakenya kuvuka na kurejeshwa.

Wakenya 23 walikuwa miongoni mwa watu 260 waliokolewa na kuruhusiwa kuvuka mpaka baada ya mpaka kufunguliwa kuokolewa kutoka kwa mikono ya maharamia.

Mmoja wa mateka hao wa kutoka Kenya aliyefanikiwa kutoroka alikiri kuwa maharamia hao wamewawateka nyara takriban watu 1,000.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *