Hussein Mohammed achaguliwa Rais mpya wa FKF,ampiga dafrao Mwendwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Hussein Mohammed ndiye Rais mpya wa Shirikisho la kandanda nchini FKF katika uchaguzi ulioandaliwa Jumamosi, baada ya kumpiga dafrao Nick Mwendwa, aliyekuwa mwaniaji mwenza wa Doris Petra.

Hussein alipata kura 62 dhidi ya 31 za Petra na Mwendwa katika raundi ya pili ya upigaji kura.

Ilibidi raundi ya pili ya upigajikura ifanyike baada ya wapinzani wote kukosa kupata idadi toshelezi ya kura kutangazwa mshindi.

Hussein alipatakura 42 dhidi ya 31 za Petra.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa FKF Barry Otieno amezoa kura 10 wakati Cleophas Shimanyula akiambulia kura 4, Sammy Owino kura 2,naye Tom Alila akapata kura moja pekee.

Waaniaji wengine Chris Amimo na Sam Ochola hawakupata kura hata moja.

Hussein pamoja na Naibu wake McDonald Mariga watahudumu kwa kipindi cha miaka minne .

Kwenye hotuba yake baada ya kuchaguliwa Hussein amabye ni Afisa Mkuu mtendaji wa shirika la Extreme Sports,ameahidi kufufua viwango vya kandanda vilivyodorora.

Nick Mwendwa alikuwa amehudumu afisinj kwa miaka minane kama Rais wa FKF.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *