Atemi Oyungu kusherehekea miaka 25 katika muziki

Mwanamuziki huyo atazindua pia albamu mpya kama sehemu ya maadhimisho hayo.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Kenya Atemi Oyungu, amepanga kusherehekea miaka 25 katika muziki na kuzindua albamu mpya.

Hafla hiyo itaandaliwa siku ya wapendanao ulimwenguni Februari 14, 2025 katika eneo la Broadwalk Residency na imepatiwa jina la “Love Unplugged” .

Albamu itakayozinduliwa siku hiyo inaitwa “Mahaba Hewani”.

Atemi aliingilia muziki mwaka 1996 na katika kipindi cha miaka 25 amejiweka katika nafasi nzuri kama mwanamuziki stadi humu nchini.

Nyimbo zake nyingi ni za mitindo ya Afro-soul na Rythm & Blues na zinapendwa sana kati ya wasikilizaji.

Amewahi kushirikiana na wanamuziki tajika humu nchini na nje akiwemo Eric Wainaina, Nikki na Lady Jaydee wa Tanzania.

Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye “Love Unplugged” ni pamoja na Wyre na Kagwe Mungai.

Albamu ya “Mahaba Hewani,” ina nyimbo 14 ambazo ni za mapenzi na hisia mbali mbali na ameshirikiana na wasanii mbali mbali.

Nyimbo hizo ni He Walks, Wivu, Close Your Eyes ambao amehisisha F-Jay, Good, In Love ambao amehusisha Wyre, Liar
na Love On Me.

Nyingine ni Kwaheri ambao amehusisha bendi ya Hart The Band, Let Him Go, Stay, Sweetie, The One, Today ambao amehusisha Kagwe Mungai na Wambura Mitaru, Yesu na Bebi Bebi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *