Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa wanawake maarufu kama Harambee Starlets, itashuka dimbani leo saa mbili usiku kumenyana na timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 23 ya Morocco nchini Morocco.
Kenya ilifanya mazoezi ya kwanza jana baada ya kuwasili, huku ikitumia mechi mbili za kujinoa makali nchini Morocco kujiandaa kwa mechi zijazo za kufuzu.
Baada ya leo Kenya chini y ukufunzi wa Beldine Odemba watarejea uwanjani kwa mechi ya pili ya kirafiki Jumanne ijayo dhidi ya wenyeji wao.
Mechi zote mbili zitachezwa katika uwanja wa Mohammed VI mjini Rabat Morocco.