Serikali ya Rwanda imekanusha shutuma zinazoelekezwa kwa jeshi lake RDF na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC.
Rwanda imesema kamwe madai hayo ni porojo na hayana msingi wowote, ikisisitiza kuwa jeshi lake la RDF lina majukumu ya kulinda mipaka ya nchi.
Kulingana na Rwanda, SADC imetuma majeshi ya kulinda amani SAMIDRC kuisadia serikali ya DRC.
Kadhalika, Rwanda imeshutumu majejeshi hayo ikisema yanashirikian na wanajeshi wa Burundi na mamluki kutoka ulaya kupigana na waasi wa M23, hali inayozorotesha usalama ziaidi.
Rwanda imeunga mkono hatua ya majadiliano ya pamoja kati ya SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, kutika jitihada za kutafuta suluhu kwa mzozo huo wa muda mrefu.