Klabu ya AFC Leopards imesajili ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Nairobi City Stars katika mojawapo wa mechi za Ligi Kuu FKF zilizosakatwa Jumapili.
Ingwe walipata bao pekee na la ushindio katika dakika ya 5 ya ngongeza kipindi cha pili kupitia kwa Kayci Odhiambo uwanjani Dandora, ukiwa ushindi wa nane msimu huu.
Kwenye matokeo mengine, wageni Bandari walisajili ushindi wa mbao 3-2 ugenini kwa Murang’a Seal, nao Police FC wakashikwa koo kwa kutoka sare ya bao moja na Sofapaka.
Shabana FC wakiwa nyumbani katika uchanjaa wa Gusii wametoka sare tasa na Kariobangi Sharks huku Tusker FC pia wakiumiza nyasi bila lengo maalum dhidi ya Kenya Commercial.