Prof. Kithure Kindiki, ataapishwa kesho Ijumaa kuwa Naibu Rais wa taifa hili, baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa mamlakani na bunge la taif na lile la Seneti.
Kupitia gazeti rasmi la serikali la tarehe Oktoba 31, 2024, hafla ya kuapishwa kwa Kindiki itaandaliwa katika Jumba la mikutano ya Kimataifa,KICC Jijini Nairobi kati ya saa nne asbuhi na saa sita adhuhuri.
“Umma unafahamishwa kuwa hafla ya kuapishwa kwa Naibu Rais mteule itaandaliwa katika jumba la mikutano ya kimataifa KICC kati ya saa nne asubuhi na saa sita adhuhuri,” ilisema gazeti rasmi la serikali.
Tangazo hilo linajiri saa chache baada ya mahakama kuu kuondoa maagizo ya kuzuia kuapishwa kwa naibu rais mteule Kithure Kindiki.
Jopo la majaji watatu likiongozwa na Justice Eric Ogola,Anthony Mrima na Dr. Freda Mugambi, lilitoa uamuzi huo leo Ijumaa likisema kuendelea kusalia wazi kwa ofisi ya naibu rais kunakiuka baadhi ya sehemu za katiba.