Ukuzaji wa Elimu Jumuishi na Usawa kupitia Mfumo Mpya wa Ufadhili (NFM) nchini Kenya

Tom Mathinji
4 Min Read

Dkt. Muchelule Yusuf, Mhadhiri Mwandamizi na Mshauri.

Mfumo Mpya wa Ufadhili (NFM) ulizinduliwa na Rais William Ruto Mei 3, 2023, baada kushirikisha umma kwa mapana na marefu, ikiwa ni pamoja na washikadau wote.

Mfumo huu unajumuisha msaada wa masomo na mikopo na ulifanyiwa marekebisho kwa kuzingatia kiwango cha uhitaji wa mwanafunzi.

Pia unaangazia changamoto ambazo vyuo vikuu vya umma na taasisi za elimu ya kiufundi(TVET) zinakumbana nazo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na taasisi hizo na ufadhili usiotosheleza.

Mfumo huu mpya wa ufadhili unachukua mahalipa ule wa kila mwanafunzi kugharimia malipo ya mpango wa masomo kwa mwaka, yaani Differentiated Unit Cost (DUC), ambao awali ulitumiwa kufadhili vyuo vikuu.

Kwa kutumia DUC, serikali ilitarajiwa kulipa asilimia 80 ya gharama ya mpango huo wa masomo, ambao kadiri muda ulivyosonga, ulikuwa umepungua hadi asilimia 35 na kuwaacha wanafunzi na vyuo vikuu kugharimia nakisi iliyotokana na upunguaji huo.

Kutokana na kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ufadhili, gharama ya mpango wa masomo inalipwa kwa asilimia 100, huku serikali ikiwalipia wanafunzi wenye mahitaji hadi asilimia 95.

Nakisi yoyote iliyosalia itagharimiwa kupitia michango ya kaya na mikopo.

Mfumo huu unatoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye uhitaji wa fedha na unatenganisha utoaji nafasi kwa wanafunzi na ufadhili.

Kipimo cha Uwezo wa Wanafunzi – MTI.

Kipimo cha Uwezo wa Wanafunzi (MTI), kitatumika kutathmini kiwango cha uhitaji kwa ajili ya kuwafadhili wanafunzi wanaotuma maombi ya msaada wa masomo katika vyuo vikuu na taasisi za TVET, ambazo kamwe hazipati ufadhili kutoka kwa mfuko wa serikali.

Ili kubaini kiwango cha uhitaji, wanafunzi wanatakiwa kutuma maombi kupitia tovuti  ambayo ni www.hef.co.ke ambapo kupitia tovuti hiyo, wanatarajiwa kutoa taarifa juu ya historia yao ya masomo na familia.

Taasisi zinazotekeleza mfumo mpya ambazo ni Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB), Mamlaka ya kutoa nafasi kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi zingine za Elimu ya Juu(KUCCPS),na Mfuko wa Vyuo Vikuu (UF), huthibitisha taarifa hizo na kuhakikisha zinalingana na data za serikali.

UF itatoa msaada wa masomo kwa wanafunzi, HELB itatoa mikopo kwa wanafunzi,na KUCCPS itasimamia utoaji wa nafasi kwa wahitimu wa mtihani wa kidato cha nne, KCSE kuanzia mwaka 2022 na kuendelea.

Zaidi ya hayo, taasisi hizo zitahudumu kama wapokeaji wa mikopo na misaada ya masomo iliyotolewa kwa wanafunzi kama karo, huku wazazi wakitoa michango ya fedha za kaya kwa ajili ya masomo ya watoto wao.

Matokeo ya MTI yanatumiwa kuwaweka wanafunzi katika makundi matano yenye viwango tofauti vya ufadhili kama ifuatavyo;

Kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo juu, wanafunzi wote waliopewa nafasi na KUCCPS wanapata ufadhili wa serikali kuanzia asilimia 60 hadi 95, chini ya mfumo mpya wa ufadhili.

Si hayo tu. Kitendo sawazishi kinatumika kwa makundi mbali mbali katika jamii huku wale wanaopewa kipaumbele wakiwa wanafunzi mayatima, wenye ulemavu na makundi yaliyotengwa.

Wanafunzi pia wanapatiwa fedha za kujikimu kimaisha za kati ya 40,000 hadi 60, 000, ambazo wanatumiwa kwa njia ya MPesa na kwenye akaunti zao za benki.

Kauli mbiu ya mfumo mpya wa ufadhili ni kuto mwacha nyuma mwanafunzi yeyote kupitia ujumuishaji na usawa.

Mfumo mpya wa ufadhili pia unatumiwa kufadhili taasisi za TVET.

Ingawa vyuo vikuu vinaweka vyenyewe gharama ya mipango yake y amasomo, kwa TVET, gharama hiyo imelinganishwa na kuwa 67, 600 kwa mwaka.

Kati ya fedha hizi, serikali inalipa kuanzia asilimia 73 hadi 92.5, na hivyo kufanya gharama ya taasisi za TVET kuwa nafuu mno.

Vile vile, wanafunzi katika  taasisi za TVET wanapokea kati ya shilingi 13, 600 hadi I8, 600 za kujikimu kimaisha.

Share This Article