Ndege ya jeshi yahusika kwenye ajali

Marion Bosire
0 Min Read

Ndege moja ndogo ya jeshi la wanahewa imeanguka jioni ya leo punde baada ya kupaa kutoka uwanja wa michezo wa Chemolingot huko Baringo.

Ndege hiyo inasemekana kugonga mti kabla ya kuanguka.

Kwenye taarifa jeshi la wanahewa la Kenya limethibitisha kwamba wote waliokuwa kwenye ndege hiyo walitoka wakiwa salama.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Nairobi wakati ajali ilitokea.

Website |  + posts
Share This Article