Boniface Mwangi, wengine 4 waachiliwa kwa dhamana

Martin Mwanje
1 Min Read

Mahakama imemwachilia huru mwanaharakati Boniface Mwangi na wenzake wanne waliokamatwa jana Alhamisi  na kushtakiwa kwa tuhuma za, miongoni mwa mambo mengine, kuchochea vurugu.

Watano hao walikamatwa wakati wakiandamana jijini Nairobi.

Mwangi na wenzake wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20,000 pesa taslimu au dhamana ya shilingi 50,000.

Upande wa mashtaka ulikuwa umeiomba mahakama kuwazuilia kwa siku 21 ili kuruhusu kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na maandamano yanayoendelea nchini.

Hata hivyo, Hakimu Mkuu Mwandamizi Gilbert Shikwe alikataa ombi hilo akisema upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi wa kutosha wa kuzuiliwa kwao.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *